Jose Mourinho ametoa kidokezo cha karibuni
zaidi kwamba Manchester United wanataka kumnunua tena Paul Pogba kutoka
Juventus ya Italia.
Mourinho amesema “mmeona moshi, jueni kuna moto”.
United
wanadaiwa kutoa £100m, ambayo ni rekodi ya dunia, kumnunua mchezaji
huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa mwenye umri wa miaka 23. Pogba aliondoka Old Trafford mwaka 2012 akiwa na umri wa miaka 19.
Manchester United walilipwa £800,000 pekee na klabu hiyo ya Italia. "Sitawafanya kuwa watu wasiojua na kutaka kuwaonesha kwamba hatujaribu kumnunua mchezaji mmoja,” amesema Mourinho.
Meneja
huyo kufikia sasa amenunua wachezaji watatu: beki Eric Bailly kutoka
Villarreal, kiungo wa kati Henrikh Mkhitaryan kutoka Borussia Dortmund
na mshambuliaji wa Sweden Zlatan Ibrahimovic.
Alipoulizwa kuhusu
uwezekano wa kumnunua Pogba, Mourinho alisema: “Tulijiwekea malengo
matatu, tulipata watatu na tutampata huyo wa nne.”
This is dummy text. It is not meant to be read. Accordingly, it is difficult to figure out when to end it. But then, this is dummy text. It is not meant to be read. Period.
ConversionConversion EmoticonEmoticon