Polisi katika mji
wa Munich nchini Ujerumani wamesema mtu aliyewapiga risasi na kuwaua
watu tisa katika eneo lenye maduka mengi siku ya Ijumaa hakuwa na
uhusiano wowote na kundi linalojiita la Islamic State.
Wanasema
kijana huyo aliyekuwa na silaha mwenye umri wa miaka 18 alizaliwa na
kulelewa Munich na alikuwa na pasipoti mbili ya Kijerumani na ya
Ki-Iran.Pia alikuwa anapata matibabu ya maradhi ya akili.
Polisi wamesema shambulio hilo lilikuwa na kila ishara ya mtu muuaji ila hamna uhusiano wowote na ugaidi.
ConversionConversion EmoticonEmoticon