Kuwa na furaha na amani katika maisha
kunachangia maendeleo kwa kiasi kikubwa kulinganisha na pale ambapo
vyote hivyo vinapokosekana. Hivyo serikali ya India imeamua kuanzisha wizara itakayo simamia na kuhakikisha wananchi wake wanakua na furaha yaani “MINISTRY OF HAPPINESS”.
Ambapo serikali hiyo imetangaza
kuwa wizara hiyo ya furaha itakuwa na majukumu ya kuhakikisha wananchi
wanakua na furaha ambapo pia itakuwa inawashauri ni namna gani
wanaweza kuishi vizuri na kwa furaha siku zote. Pia itasisitiza juu ya
kufanya mazoezi ya ku relax “YOGA” mafundisho ya kiroho ili kupunguza msongo wa mawazo.
Jimbo la Mandya Pradesh
ambapo ndipo idea ama wazo lilipozinduliwa, ni moja kati ya maeneo
ambayo maendeleo sio makubwa nchini India na kuna kiwango kikubwa cha
mauaji binafsi kwa watoto na wakulima kutokana na ugumu wa maisha.
Licha ya hayo yote pia jimbo hilo lililopo katikati ya India
linaongoza kwa mauaji ya watoto wachanga na matukio ya ubakaji.
Serikali ya India inaamini kwa kuanzisha wizara ya furaha, haya yote
yatapungua.
ConversionConversion EmoticonEmoticon