Rais Magufuli atishia kubadili noti



September Mosi 2016 Rais Magufuli amezungumza katika mkutano wa 14 wa mwaka wa wahandisi uliofanyika katika ukumbi wa mlimani City jijini Dar es salaam.
Katika kile kinachoonekana ni kutaka kuwadhibiti watu wanaodaiwa kuficha fedha, Rais Magufuli amesema kuwa mamlaka aliyonayo anaweza kuamua kubadili fedha ili zile zinazofichwa na watu hao wakose mahali pa kuzipeleka.
Aidha amesisitiza kuwa katika utawala wake fedha za bure hazitakuwepo kwa sababu zilikuwepo awali zilitokana na fedha za wizi kutoka serikalini ambazo kwa sasa zimedhibitwa, alisema kwa mwendo anaokwenda nao sasa sasa ni ngumu kwa mwananchi kupata fedha bila kufanya kazi
Previous
Next Post »