Shirikisho la Mpira
Miguu Tanzania limemteua Sebastian Nkoma kuwa Kocha Mkuu wa timu ya
soka taifa ya wanawake wa Tanzania Bara maarufu kwa jina la Kilimanjaro
Queens.
Kilimanjaro Queens kwa mara ya kwanza inakwenda kushiriki
mashindano ya kuwania Kombe la Afrika Mashariki na Kati yatakayofanyika
kwa siku tisa kuanzia Septemba 11, jijini Jinja Uganda.Uteuzi huo wa Nkoma unakwenda sambamba na wasaidizi wake, ambao ni Hilda Masanche na Edna Lema wakati Meneja wa timu hiyo, Furaha Francis, Mtunza vifaa ni Esther Chabruma.
Timu hiyo itasafiri kwenda Uganda jumatatu kupitia Bukoba mkoani Kagera itakakoweka kambi tena ya siku nne.
Ikiwa mkoani Kagera itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi ambayo pia itakuwa njiani kwenda Uganda kwenye mashindano hayo yanayoratibiwa na baraza la Vyama vya mpira wa miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Tanzania itacheza michezo wake wa kwanza dhidi ya Rwanda Septemba 12, kabla ya kucheza na Ethiopia Septemba 16.
Rwanda na Ethiopia zitacheza Septemba 14, wakati kundi A Zanzibar itakata utepe kwa kucheza na Burundi na siku hiyohiyo, Uganda itacheza na Kenya.
ConversionConversion EmoticonEmoticon