Familia
ya “Rais Mteule” wa Marekani Donald Trump inazidi kuzimiliki headlines
kubwa wakati ikijiaandaa kuingia Ikulu ya White House. Mbali na nafasi
aliyoipata mfanyabiashara huyo tajiri, Trump anaishi maisha ya kifahari
kwenye jumba lake lenye thamani ya shilingi za Tanzania zaidi ya Bilioni
215.
Jumba
hilo liko kwenye eneo lenye ukubwa futi za mraba elfu themanini
(80,000) ufukweni mwa jiji la Florida. Trump alinunua jumba hilo kwa
dola za Marekani Milioni 5 mwaka 1985 na kulifanyia ukarabati ambapo
sasa lina vyumba vya kulala 58, bafu 33, jiko lenye meza za Marble kwa
ukubwa wa futi 29, pamoja na sehemu za kuwasha moto 12.
ConversionConversion EmoticonEmoticon