Imetokea Brazil na Mwanamke mwenyewe anaitwa Vera Lucia da Silva
na umri wake ni miaka 44 ambapo aliamua kukaa kwenye jeneza siku nzima
ili apate uzoefu wa mazingira ya kifo ili siku akifa asiwe mgeni na
Jeneza.
Vera
aliamua kukaa kwenye jeneza huku familia yake ikifanya vitu vinayofanywa
kwenye msiba ili aone inakuaje ambapo baada ya kutoka humo alisema
ilikua siku nzuri zaidi kwenye maisha yake yote.
Sherehe
hiyo ya kujifunza maisha ya kwenye Jeneza ambayo ilifanyika Jumatano
ya November 2 2016 ni sherehe ambayo ilifanyika kwenye eneo la makaburi.
Ndugu zake
walipingana sana na wazo lake lakini baadae waliamua kukubaliana naye
na kuvaa nguo nyeusi wakati walipomtembelea na kufanya kama wanatoa
heshima za mwisho.
Mmiliku wa
eneo la kuzikia liitwalo Eternal Garden Funeral home, Paulo Araujo,
aliamua kumpa Jeneza Vera bila gharama zozote, kama mgeni maalumu.
Wakati akiwa ndani ya Jeneza mwanamke huyo alikua akifumbua macho na kufumba kama vile mtu aliyekufa na kufufuka.
Mwanamke
huyo amesema alikuwa na ndoto ya kulala kwenye Jeneza tangu miaka 14
iliyopita na hakuwa akifikiri ingekuja kutokea akaitimiza, kwasasa
amefurahi kutimiza alichokitaka kabla hajafa
ConversionConversion EmoticonEmoticon