Maneno ya Jose Mourinho baada ya Rooney kunaswa kalewa

November 16 2016 nahodha wa timu ya taifa ya England na klabu ya Man United Wayne Rooney alitolewa kwenye gazeti la The Sun akionekana kalewa huku akiwa na wadada, Rooney kanaswa na The Sun katika picha akiwa kalewa akiwa kavaa mavazi ya timu ya taifa.
Stori kutoka kwenye gazeti la The Sun limemtoa Rooney ukurasa wa mbele huku likieleza kuwa staa huyo amenaswa akiwa katika sherehe ya harusi, baada ya picha hizo kuenea kocha wa Man United Jose Mourinho amewalaumu viongozi wa FA kwa kitendo cha kumruhusu Rooney kulewa.
rooney-drunk
Mourinho ameonekana kuwalaumu zaidi viongozi wa chama cha soka cha England FAna sio Rooney kutokana na gazeti la The Sun kuwataja viongozi FA kuwa ndio walikuwepo katika harusi hiyo, Mourinho hawezi kuelewa kambi ya timu ya taifa ya England inavyoendeshwa.
Previous
Next Post »