Aliyekuwa
askari wa Jeshi la Polisi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, Kuyani
Mkunjera (36), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Moshi,
kwa kupokea mshahara wa jeshi hilo huku akiwa ameacha kazi kwa kipindi
cha miezi saba.
Hakimu
mkazi wa mahakama hiyo, Antony Ngowi alisema mshtakiwa alijinufaisha
pasipo kufanyia kazi kitu anachonufaika nacho na alipokea fedha kiasi
kinachozidi Sh4.6 milioni ambayo ni kinyume cha kifungu cha 23 (1) (a)
cha Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Sheria namba 11 ya mwaka 2007.
Ngowi
alisema mshtakiwa kuanzia Oktoba 12, 2015 hadi Aprili 28, mwaka huu
alijipatia kiasi hicho cha fedha kwa kujinufaisha pasipo kukifanyia kazi
kitu anachonufaika nacho, huku akiwa siyo mfanyakazi wa jeshi hilo na
akiwa ameajiriwa na taasisi nyingine.
Mshtakiwa
alikana shitaka hilo na yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti
yaliyomtaka awe na kiasi cha Sh3 milioni za ahadi na wadhamini wawili
wenye barua za kuwatambulisha, vitambulisho na picha za paspoti.
ConversionConversion EmoticonEmoticon