Ni
rasmi! Straika wa Yanga, Malimi Busungu, ataikosa michezo yote ya msimu
huu iliyobakia ya timu hiyo baada ya kuvunjika mbavu za upande wa
kushoto katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Sagrada
Esperanca ya Angola na kushauriwa kupumzika kwa zaidi ya wiki nne, sawa
na mwezi mmoja.
Busungu
ambaye katika mchezo huo alianza kikosi cha kwanza, hakuweza kumaliza
dakika zote baada ya kuumia dakika ya 53 na nafasi yake kuchukuliwa na
Geofrey Mwashiuya.
Baada
ya kuumia, Busungu alikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke kwa
ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kina kutokana na marejaha hayo ambayo
yalitokana na kugongwa na kipa wa Esperanca, Yuri Jose Tavazes.
Mshambuliaji
huyo mwenye mabao mawili katika Ligi Kuu Bara msimu huu, ataikosa
michezo mitatu ya ligi hiyo ambayo ni dhidi ya Mbeya City, Ndanda na
Majimaji, huku pia akiukosa mchezo wa marudiano dhidi ya Esperanca
utakopigwa Mei 17, Mwaka huu nchini Angola.
ConversionConversion EmoticonEmoticon