Kampuni ya Gucci imepigwa marufuku kutumia tangazo moja nchini Uingereza ambalo linamuonyesha mrembo mmoja aliyedhoofika kiafya.
Mamlaka ya viwango vya matangazo imeamua kwamba vile alivyosimama mwanamke huyo pamoja na alivyojipodoa kunamuweka aonekane kama aliyeathirika kutokana na ukosefu wa mlo.
Mamlaka hiyo imesema kuwa ilibaini kwamba kiwiliwili cha mwanamitindo huyo pamoja na mikono yake ilikuwa myembamba na haikuwa sawa na kichwa na eneo la chini la mwili wake.
”Pia tulibaini kwamba hisia za uso wake na vipodozi vyake vyeusi alivyopakwa hususan kandokando ya macho yake vinamfanya kuonekana aliyedhoofika.Kwa sababu hizo tumeamua kwamba mwanamitindo huyo aliyekuwa anategemea ukuta amedhoofika kiafya na kwamba tangazo hilo halina uwajibikaji,” ilisema mamlaka hiyo.
ConversionConversion EmoticonEmoticon