Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa amewachwa nje katika kikosi cha Uhispania cha Euro 2016.
Kocha
Vicente del Bosque pia amemwacha nje kiungo wa kati wa Manchester
United Juan Mata pamoja na aliyekuwa mshambuliaji wa Liverpool na
Chelsea Fernando Torres.Mabingwa watetezi, Uhispania wako katika kundi D pamoja na Croatia,Czech na Uturuki wakiwania taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo.
Costa amefunga bao moja katika mechi 10 kwa Uhispania.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alikosa kucheza mechi mbili za mwisho za klabu yake Chelsea kutokana na jeraha la mguu.
Beki wa Bayern Munich Javi Martinez ,kiungo wa kati wa Arsenal Santi Carzola pia wamewachwa nje huku kocha Del Bsoque akimshirikisha Saul Niguez wa Atletico Madrid na Lucas Vazquez wa Real Madrid.
Wachezaji wa ligi ya Uingereza katika kikosi hicho ni mlinda lango David de Gea,wachezaji watatu wa Chelsea; Pedro,Cezar Azpilicueta na Cesc Fabregas pamoja na kiungo wa kati wa Manchester City David Silva.
ConversionConversion EmoticonEmoticon