Wabunifu wakomavu na chipukizi wanaonyesha mitindo yao katika maonyesho ya mitindo ya kiafrika mjini London wiki hii.
Lakini
katika enzi ambapo wanablogu wa mitindo wanaotumia video kuonyesha
mitindo yao, mwandishi wa BBC Alexis Akwagyiram anatathmini ikiwa
darubini imehamishwa kutoka kumbi za maonyesho hadi katika mitandao ya
kijamii.Ulingo wa fasheni umejaa picha za wanamitindo warembo wanaotembea katika kumbi za fasheni wakiwa wamevalia nguo za kupendeza zenye mitindo mbali mbali.
Maonyesho kama hayo ndio yanayoshuhudiwa katika maonyeso ya kila mwaka mjini London hii ikiwa mara yake ya nne.
"Afrika kwa sasa inang'aa," asema Josette Matomby, msimamizi wa maonyesho kutoka DRC ambae pia ni mbunifu anayeishi London. Yeye pia ni mmoja wa waasisi wa maonyesho haya ya London.
Anataja kampuni ya Vlisco ya uholanzi kama moja ya kampuni zenye kueneza mitindo ya kiafrika.
Bi Matomby anasema nguo za kiafrika zimeanza kuwika katika ulingo wa kimataifa katika miaka ya hivi karibuni na hata kuvutia kampuni kubwa za mitindo kama vile Burberry.
Hofu kwamba, wabunifu wa kiafrika hawakuwa wakifaidi kutokana na kazi zao ilikua sehemu ya msukumo wao wa kuanzisha maonyesho kama haya ya kupigia debe mitindo yao Afrika na ughaibuni.
ConversionConversion EmoticonEmoticon