Hii ni kwa mujibu wa duru za polisi na afya.Shambulio hilo lilitokea mji wa Sadr ulio na waumini wengi wa Ki-Shia wakati wa asubuhi kukiwa na shughuli nyingi.
Wapiganaji wa Islamic State{IS} wamekiri kuhusika na shambulio hilo na kusema lilinuia kulenga kundi la wapiganaji wa Ki-Shia.
Wapiganaji wa IS ambao ni waumini wa Sunni wanadhibiti Magharibi na Kaskazini mwa Iraq.
Wamekua wakiwalenga waumini wa Shia ambao wanawataja kuwa kafiri.Hata hivyo hii leo waathiriwa wengi walikua wanawake na watoto.
Shambulizi hilo liliharibu kabisa majengo na magari yaliyokua karibu. Kundi la IS limekua likilenga maeneo ya biashara nchini Iraq.
Mnamo mwezi Februari takriban watu 70 waliuawa katika misururu miwili ya mashambulizi ya bomu katika soko lililoko mji wa Sadr. Shambulio hilo lilitajwa kuwa baya zaidi kutokea mjini Baghdad kwa miezi.
Wanajeshi wa Iraq wakisaidiwa na mashambulizi ya anga ya Marekani pamoja na wapiganji wa Kishia wameweza kuyakomboa maeneo kadhaa kutoka kwa IS, lakini kundi hilo limeweza kushambulia mji mkuu
ConversionConversion EmoticonEmoticon