Taasisi
ya kuzuia na Kupambana na rushwa (TAKUKURU) imebaini kuwepo kwa sukari
iliyofichwa tani 4,579.2 iliyonunuliwa toka Kiwanda cha Sukari
Kilombero.
Kwa
mujibu wa Taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi
Mkuu wa TAKUKURU Valentine Mlolowa Taasisi hiyo imeanza uchunguzi dhidi
ya swala hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.
Taarifa
hiyo imefafanua kuwa mnamo tarehe 05 Mei, 2016 timu ya uchunguzi
ilitembelea maghala yaliyopo Tabata Jijini Dar es salaam na kubaini
uwepo wa sukari hiyo.
TAKUKURU
tayari imetembelea Maghala ya mfanyabiasha Haruni Daudi Zacharia
ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Al-Naeem yaliyoko Mbagala na Tabata
ambaye ni miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa wa sukari hapa nchini na
anayetuhumiwa kuficha bidhaa hiyo.
Aidha
uchunguzi uliofanywa na Taasisi hiyo ulibaini kuwepo kwa njama za
dhati za kutouza sukari iliyokutwa katika maghala hayo kulikofanywa na
mfanyabiashara huyo kwani hata sehemu ya Maghala ilipo sukari hiyo
hapakuwa na dalili za upakiaji wa sukari hiyo ili iweze kusambazwa.
Taarifa
hiyo imeendelea kufafanua kuwa katika eneo la Kitumbini kumekuwa na
wananchi wengi wanaohitaji bidhaa hiyo na wachache sana waliweza
kuuziwa licha ya ukweli kwamba sukari ilikuwepo.
Katika
uchunguzi wake TAKUKURU pia imebaini kuwepo kwa mikakati ya dhati
iliyokuwa ikifanywa na mfanyabiasha huyo kwa kununua sukari yote toka
viwanda vya ndani na kisha kuihifadhi na kuuza bidhaa hiyo kidogo kidogo
kwa wastani wa tani 250 kwa siku wakati alikuwa na uwezo wa kuuza zaidi
jambo lililochangia uhaba wa sukari katika soko.
Kuficha
bidhaa ni kosa la uhujumu uchumi na ni kinyume na Aya ya 3 Jedwali la
kwanza Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 [Chapisho la Mwaka 2002].
Serikali haitavumilia hujuma za namna hii na itachukua hatua kali dhidi
ya mfanyabiashara yeyote ataekwenda kinyume na sheria hii.
TAKUKURU
inatoa wito kwa wafanyabiashara wote wa sukari kuacha vitendo vya
kuficha sukari na vyombo vya uchunguzi vinafuatilia kote nchini na
yeyote atakayebainika kufanya hujuma hizo atakabiliwa na mkondo wa
Sheria.
ConversionConversion EmoticonEmoticon