Kiongozi wa mkuu wa Taleban auawa


Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa:
Serikali ya Afghanistan pamoja na kamanda mwandamizi wa kundi la Taliban wamethibitisha kuuawa kwa kiongozi wa kundi hilo la waislamu wa dhehebu la Sunni wahabia lenye makao makuu Saudia arabia, Mullah Mohammed Akhtar Mansour, kufuatia shambulizi lilofanywa na Marekani kwa kutumia ndege isiyokuwa na rubani.
Shambulizi la aina hiyo ni la kwanza kutokea katika eneo la Baluchistan lilioko katika mpaka baina ya Pakistan na Afghanistan. Na huenda ikawa ndio sababu ya Mansour kuwa safarini bila ya ulinzi. Aidha waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry akiwa ziarani nchini Myanmar amesema, Mansour alikuwa ni kitisho kikubwa kwa wafanyakazi wa Kimarekani walioko Afghanistan, raia wa Afghanistan, pamoja na vikosi vya usalama nchini humo. Ameongeza kuwa shambulizi dhidi ya Mansour ni ujumbe kwa dunia ya kwamba Marekani itaendelea kushirikiana na Afghanistan katika mchakato wake wa kutafuta amani.e55871706bcc06072822399d90218e73
Previous
Next Post »