ASHA Rose Migiro, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN),
muda wowote kuanzia sasa, atatangazwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini
Uingereza. Taarifa za ndani kutoka katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa zinaeleza kuwa,
jina la Dk. Migiro ambaye aliwahi kutumikia nafasi mbalimba ndani na nje
tayari limefikishwa Uingereza kwa zaidi ya mwezi mmoja uliopita.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya Februari mwaka huu Rais John Magufuli kutangaza kwamba, Dk. Migoro atateuliwa kuwa balozi bila kutaja nchi atakayokwenda kuiwakilisha Tanzania.
Uteuzi wa Dk. Migoro uliibua mjadala kutokana na kushika kwake nafasi mbalimbali za kidiplomasia ambapo mjadala huo ulijielekeza kuwa ‘ameshuka ama amepanda?’
Miongoni mwa nafasi za juu za kidiplomasia alizowahi kushika Dk. Migiro ni pamona na kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN).
Aliteuliwa tarehe 5 Januari 2007. Dk. Migiro aliteuliwa na Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) kushika nafasi hiyo akiwa mwanamke wa pili kushika wadhifa huo baada ya Louise Fréchette, mwanadiplomasia wa Canada aliyeongoza kuanzia Aprili 1997 hadi Aprili 2006.
Dk. Migiro alichukua nafasi hiyo iliyoachwa na George Mark Malloch Brown wa Uingereza. Dk. Migiro alishikilia wadhifa huo kwa miaka mitano. Julai 2012 nafasi yake ilichukuliwa na mwanadiplomasia wa Sweden, Jan Elliason

ConversionConversion EmoticonEmoticon