Beyonce Giselle Knowles ameifungulia
mashtaka kampuni ya Feyonce Inc ya Texas pamoja na watu watatu kwa kuuza
bidhaa kwenye mtandao wao wa intaneti kwa kutumia jina la “Feyonce”.
Mwimbaji huyo nyota wa muziki wa pop
aliye maarufu na ushawishi mkubwa duniani, ameitaka mahakama kuizuia
kampuni hiyo ya kuuza mavazi ya aina mbalimbali yakiwamo mashati na
vikombe vya kahawa ikitumia jina hilo.
Beyone anadai kuwa bidhaa hizo zenye jina
la Feyonce, linakaribiana sana na jina lake la kibiashara la Beyonce,
kwani kwa kufanya hivyo ni kumharibia jina lake ambapo ni brand yake.
Miongoni mwa bidhaa hizo ni kikombe
kikubwa kinachouzwa dola 14.95 chenye maneno “he put a ring on it,”
ambayo Beyonce, amedai yamewekwa kwa lengo maalumu kwani yanatoka katika
mashairi ya wimbo wake ‘Single Ladies’.
Mke huyo wa rapa Jay Z, amesema uuzaji wa
bidhaa hizo za Feyonce ni ulaghai wa makusudi ambao unawachanganya
wanunuzi na kusababisha madhara kwake.
ConversionConversion EmoticonEmoticon