Bajeti wizara tatu wiki hii, imo ya Habari

MKUTANO wa tatu wa Bunge la 11 unaendelea tena leo mjini Dodoma, na wiki hii, Serikali itawasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka wa fedha wa 2016/17 ya wizara tatu, ikiwemo bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Ratiba mpya iliyotolewa wiki iliyopita inaonesha wizara nyingine zitakazowasilisha bajeti zao wiki hii ni Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto itakayojadiliwa kwa siku mbili.
Mwaka jana, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (wakati huo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo) ilitengewa jumla ya Sh bilioni 29.4 kati ya hizo Sh bilioni tano zilikuwa ni fedha za maendeleo na Sh bilioni 24.4 za matumizi ya kawaida.
Kwa upande wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, bajeti iliyopita, ilitengewa Sh bilioni 1.7 kwa ajili ya Matumizi ya kawaida na matumizi ya maendeleo ili iweze kutekeleza majukumu yake katika mwaka 2015/16.
Kati ya fedha hizo Sh bilioni 1.4 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Sh milioni 239.1 ni kwa ajili ya Matumizi ya Maendeleo. Kwa upande wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambayo kwa muda mrefu , bajeti imekuwa ikilalamikiwa kuwa ndogo, imejumuisha wizara mbili ya Afya pamoja na ile ya Jinsia, Jamii na Watoto
Previous
Next Post »