Wapinzani wa Simba, Yanga ndiyo mabingwa kwa mara ya pili mfululizo baada ya kufikisha pointi 71, ambazo haziwezi kufikiwa na timu za Azam inayoshika nafasi ya pili na pointi 60 wala Simba iliyopo nafasi ya tatu kabla ya mchezo wa jana jioni dhidi ya Majimaji wakiwa na pointi 58.
Akizungumza na gazeti hili Poppe, alisema wametenga kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya usajili na baada ya kutofurahishwa na mwenendo wao wa msimu huu, tayari wameanza mikakati ya kukijenga upya kikosi kitakachorudisha heshima ya Simba.
“Najua tunapata lawama kubwa kutoka kwa mashabiki na wanachama, lakini kwa kuwa sisi ndio viongozi hatuna namna ya kuzikwepa ingawa nasi tunaumizwa na matokeo…ili kurekebisha hali, tumeamua kuja kivingine msimu ujao kwa kusajili wachezaji wenye viwango vya kuichezea Simba ili tuweze kufanya vizuri,” alisema Hans poppe.
Amekiri kuwa, walikuwa na nafasi nzuri ya kufanya vyema katika ligi, lakini vipigo kutoka kwa watani wa Yanga pia vimechangia kuwavuruga, achilia mbali baadhi ya wachezaji kushindwa kuwajibika ipasavyo.
ConversionConversion EmoticonEmoticon