Mgombea urais wa
chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amesema yuko tayari
kufanya mazungumzo na kiongozi wa Korea Kaskazini kuhusu mpango wa
nyuklia wa taifa hilo.
“Ninaweza nikazungumza naye, Siwezi kuwa na tatizo kuzungumza naye,” Bw Trump alisema kuhusu Kim Jong-un.Mkutano huo ungekuwa tofauti kabisa na msimamo wa muda mrefu wa Marekani kuhusu Korea Kaskazini.
Hatua hiyo imemfanya mgombea anayeongoza katika kinyang’anyiro cha chama cha Democratic Hillary Clinton kumshutumu Bw Trump na kusema anashangaza kwa kuwaenzi sana viongozi wababe wan chi za nje.
Taarifa iliyotolewa na mmoja wa wasaidizi wa Bi Clinton imesema sera ya mambo ya nje ya Bw Trump usio wa maana yoyote.
- Obama: Trump haelewi sera za kigeni
- Trump achekwa kwa alivyotamka Tanzania
- Trump: Meya Mwislamu anakaribishwa Marekani
Wanadiplomasia wanatarajia ziara hiyo ifanyike baada yake kuwa rasmi mgombea urais wa chama cha Republican mwezi Julai.
Mapema wiki hii, Bw Trump alisema dalili zinaonesha huenda asiwe na uhusiano mwema sana na Uingereza.
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron na meya mpya wa London Sadiq Khan, ambaye ni Mwislamu, wamemshutumu Bw Trump kutokana na hatua yake ya kupendekeza Waislamu wazuiwe kuingia Marekani
ConversionConversion EmoticonEmoticon