Ulingo wa kimataifa'


Mitandao ya kijamii bila shaka imewasaidia wabunifu wa Afrika kujulikana na kusifika katika maonyesho ya kimataifa ya mitindo , wengi wanaona hili kuwa demokrasia katika sekta ya mitindo.
Mitindo ya kiafrika zamani ilionekana kama ya waafrika pekee lakini mtu yeyote mwenye tamaa ya kupata mitindo ya kiafrika anaweza kuipata kwa njia yoyote, njia kuu ikiwa kupitia hiyo mitandao ya kijamii ikilinganishwa na siku za nyuma.
Katika siku za usoni, itakuwa muhimu na lazima kwa wabunifu wa mitindo kuwa na akaunti zao kwenye mitandao ya kijamii kuweza kuionyesha kwa dunia nzima na pia ili kuweza kupata wateja.
Bado kuna nafasi kwa maonyesho ya mitindo ya Afrika , bado kuna nafasi hiyo kwa sababu hii inawapa nafasi wabunifu kuonyesha mitindo yao kwa kuwavalisha wanamitindo nguo na vitambaa vyenye mvuto na hata kuwafunza watu namna ya kuvalia nguo hizo.
Lakini kutakuwa na wakati, ambapo kutakuwa na maonyesho mengi ya mitindo ya kiafrika.
Maonyesho hayo pia hufanyika mjini Berlin na New York, na hata katika sehemu zingine katika bara la Afrika
Previous
Next Post »