Majaliwa kumwakilisha Rais mkutano wa kupiga vita rushwa


WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ataongoza ujumbe wa Tanzania utakaoshiriki kwenye mkutano wa wakuu wa nchi unaojadili suala la kupambana na rushwa utakaofanyika kesho mjini London, Uingereza.
Watakaoongozana na Waziri Mkuu ni pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kimataifa na Kikanda, Balozi Augustine Mahiga, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Valentino Mlowola, wataalamu wa sekta ya kupambana na rushwa na wanasheria.
Waziri Mkuu Majaliwa alisema Serikali ya Tanzania imeweka mkakati endelevu wa kupambana na walarushwa na imekuwa ikungwa mkono na mataifa ya nje na ndio maana Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameroon amemualika kuhudhuria mkutano huo.
“Waziri Mkuu wa Uingereza ameandaa mkutano huu na alimualika Rais Magufuli ili ahudhurie akiwa ni miongoni wa wakuu wa nchi 60 watakaohudhuria mkutano huo. Tanzania ni miongoni mwa nchi mbili kutoka bara la Afrika ambazo zimealikwa kushiriki.
Nchi nyingine ya kutoka Afrika ni Nigeria,” alisema Majaliwa. Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema kutokana na Rais kuwa na majukumu mengine atamwakilisha katika mkutano huo ambao viongozi hao watajadili na kueleza mikakati yao ya namna wanavyokabiliana na rushwa na ufisadi
Previous
Next Post »