Wanaume wawili
wanaosema kuwa maafisa wa polisi wa Kenya waliwalazimisha kufanyiwa
ukaguzi wa tupu ya nyuma ili kubaini kwamba walishiriki katika ngono ya
mapenzi ya jinsia moja wameanzisha kesi mahakamani wakitaka ukaguzi huo
kuwa ukiukaji wa katiba.
Wanasema kuwa walilazimishwa kufanyiwa
ukaguzi wa magonjwa ya virusi vya ukimwi na Hepatitis kufuatia kukamatwa
kwao mnamo mwezi Februari 2015 baada ya kushukiwa kwamba wanashiriki
katika ngono ya mapenzi ya jinsia moja.Vitendo vya wapenzi wa jinsia moja kushiriki ngono ni kinyume na sheria nchini Kenya na adhabu ya makosa hayo ni miaka 14 jela.
Mahakama ya Mombasa imewapatia mawakili wa serikali wiki moja kutoa jibu.
Chini ya sheria ya kimataifa ,ukaguzi wa lazima katika tupu ya nyuma ni kitendo cha kikatili,unyama na ni sawa na mateso kulingana na kundi la haki za kibinaadamu Human Wrights Watch
ConversionConversion EmoticonEmoticon