Jurgen Klopp: Nakubali nilikosea kuhusu Basel


 
 
Klopp
 
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema anajutia kuwaambia mashabiki wa klabu hiyo, hata wasio na tiketi, wajiandae kwenda Basel kutazama fainali ya Europa League.
Liverpool wametengewa tiketi 10,236 pekee kwa ajili ya fainali hiyo ya 18 Mei dhidi ya mabingwa watetezi Sevilla nchini Uswizi.
Klopp amesema: "Mara yangu ya mwisho kuzungumza kuhusu Basel, nilizungumza kama shabiki na kuwaalika mashabiki wote wa Liverpool mjini Basel.
“Sikutumia busara, kusema kweli. Mji wa Basel ni mzuri sana lakini hauko tayari (kutupokea sote) na hilo lilikuwa kosa langu.”
Amesema ni mashabiki wenye tiketi pekee wanaofaa kusafiri.
Uefa imelazimika kutetea uamuzi wake wa kuandaa fainali hiyo katika uwanja St Jakob-Park, unaotoshea mashabiki 35,000 pekee
Previous
Next Post »