Na Selemani Abeid, Shinyanga
WAMEKAA! Baada ya kuhangaika kwa muda mrefu, hatimaye Simba wamefanikiwa
kuongoza Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya kwanza baada ya jana
kuichapa Stand United kwa bao 2-1 mchezo uliopigwa Uwanja wa Kambarage,
Shinyanga.
Bao la Simba lililowafanya wakae kileleni liliwekwa kimiani na Hamis
Kiiza dakika ya 34, baada ya kupata pande safi kutoka kwa Ramadhan
Kessy.
Hii ilitokana na Simba kugongeana pasi safi, kabla ya kumkuta Kessy
aliyemimina krosi maridadi kwa Kiiza aliyemchungulia golikipa Frank
Muwonge na kumtungua.
Dakika ya 51, Kiiza kwa mara nyingine aliifungia Simba bao la pili
kutokana na juhudi zake binafsi.
Hilo linakuwa bao la 16 kwa Kiiza, ambaye sasa ndiye anayeongoza kwa
mabao akifuatiwa na Amisi Tambwe wa Yanga aliye na mabao 14.
Ushindi huo, umeifanya pia Simba ikae kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu
ikiwa na pointi 45, wakifuatiwa na Yanga walio na pointi 43, huku Azam
ikiwa na pointi 44.
Azam wanaweza kusogea nafasi ya pili kama watashinda katika mchezo wa
leo dhidi ya Coastal Union utakaopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani,
Tanga.
Mchezo huo ulikuwa na kosakosa kadhaa, lakini nafasi ambazo Simba
watazijutia ni ile ya dakika ya 49, pale Ibrahim Hajib aliposhindwa
kufunga akiwa amebaki na lango.
Kiiza pia alipoteza nafasi nzuri ya kufunga dakika ya 37, baada ya
kupewa pasi safi na Said Ndemla na kushindwa kulenga lango.
Stand United: Frank Muwonge, Revocatus Richard, Seleman Mrisho, Nassor
Masoud, David Osman, Jacob Massawe, Pastory Athanas, Amri Kiemba, Elius
Maguli, Seleman Salembe, Vitalis Mayanga.
Simba: Vicent Angaban, Hassan Kessy, Emery Nimubona, Abdi Banda, Juuko
Murshid, Justice Majabvi, Mwinyi Kazimoto, Jonas Mkude, Hamis Kiiza,
Ibrahim Ajib, Said Ndemla
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
ConversionConversion EmoticonEmoticon