Leo Nov 1 2016 katika Bandari ya Dar es salaam
kumetokea moto ambao umezua taharuki kwa baadhi ya wafanyakazi na watu
wengine waliokuwa eneo hilo la bandari. Moto huo uliolipuka kwenye
makontena na kuteketeza kontena tatu zilizokuwa na matairi ya magari na
kudumu kwa muda wa dakika 30.
Mkuu wa mawasiliano wa mamlaka ya Bandari, Peter Mlanzi ametoa ufafanuzi kuhusu moto huo kwamba umeandaliwa makusudi kwa ajili ya kukipima kikosi cha zima moto…….>>>’tukio
hili tumelitengeza kwa makusudi ili tuone namna ambavyo kikosi kazi
cha zimamoto na uokoaji kinavyoweza kukabilana na majanga mbalimbali’
Aidha kwa upande wake mkuu wa kikosi cha zimamoto bandari ya Dar es salaam, Mussa Biboze, amesema…..>>>’kwa zimamoto moto uko kwenye madaraja, huu moto wa matairi ni moto wa daraja A ambao unazimwa tu na maji ya kawaida‘
ConversionConversion EmoticonEmoticon