Usiku wa Septemba 21 2016 michezo ya Ligi Kuu Hispania
iliendelea kama kawaida, moja kati ya mchezo uliochezwa usiku wa
Septemba 21 na kuvuta hisia za mashabiki wengi ni mchezo kati ya FC Barcelona dhidi ya Atletico Madrid uliochezwa katika dimba la Nou Camp.
Katika mchezo huo ambao mchezaji tegemezi wa FC Barcelona Lionel Messi alitolewa nje dakika ya 51 baada ya kuumia, mchezo ulimalizika kwa FC Barcelona kulazimishwa sare ya goli 1-1, Barcelona ndio walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 41 kupitia kwa Ivan Rakitic na baadae Atletico Madrid wakasawazisha dakika ya 61 kupitia kwa Angel Correa.
FC Barcelona ambao
walikuwa wanamiliki mpira kwa asilimia 70 kufuatia matokeo sasa wanakuwa
nafasi ya tatu kwa kufikisha jumla ya point 10, wakati Atletico wakiwa nafasi ya pili kwa kuwa na point 11 na Real Madrid wanaongoza Ligi hiyo kwa kuwa na point 13.
ConversionConversion EmoticonEmoticon