Obama: Waliohusika na jaribio la mapinduzi Uturuki kushtakiwa


Rais Recep Tayyip Erdogan na mwenzake Barack Obama wa Marekani
Image captionRais Recep Tayyip Erdogan na mwenzake Barack Obama wa Marekani
Rais wa Marekani Barrack Obama anasema kuwa atahakikisha kuwa wale waliohusika na jaribio la mapinduzi nchini Uturuki watashtakiwa.
Alikuwa akizungumza alipokutana na rais Recep Tayyip Erdogan kandokando ya mkutano wa G-20 mjini Hangzhou nchini China.
Uturuki inadai kuwa kiongozi wa dini mwenye makao yake huko Marekani Fethullah Gulen ndiye aliyepanga njama ya mapinduzi hayo na inataka arudishwe nchini Uturuki.
Kiongozi wa dini kutoka Uturuki Fethullah Gulen
Image captionKiongozi wa dini kutoka Uturuki Fethullah Gulen
Lakini rais Obama hakuzungumzia kuhusu swala la kumrudisha Uturuki kiongozi huyo.
Bwana Gulen amekana kuhusika na jaribio hilo.Rais Obama na Erdogan pia walizungumzia kuhusu hali ilivyo nchini Syria.
Previous
Next Post »