Daktari apatikana na video ya watu wakishiriki ngono na nyoka

Mizani ya Haki

Daktari mmoja nchini Uingereza amepatikana na hatia ya kuwa na video za ngono, ikiwemo moja ya mwanamume akishiriki ngono na nyoka.
Cyprian Okoro, 55, kutoka kusini magharibi mwa London alipatikana na makosa matano ya kuwa na video za ngono ya kuchukiza zaidi pamoja na picha moja ya utupu ya mtoto.
Okoro amepewa dhamana lakini atahukumiwa tarehe 30 Septemba.
Kwenye moja ya video hizo, kulikuwa na wanawake wakishiriki ngono na mbwa na nyingine ya mwanamke akifanya ngono na farasi.
Mshtakiwa, ambaye anatoka Cameron Place, Streatham, alikanusha mashtaka hayo.
Lakini, baada ya kutafakari kuhusu kesi yake kwa chini ya siku moja, baraza la wazee wa mahakama lilimpata na hatia kuhusia na mashtaka yote ila lile la watu ksuhiriki ngono na mbwa.
Mahakama iliambiwa kwamba Okoro alikuwa na picha na video hizo kwenye simu yake baada ya kuzipokea kupitia WhatsApp.
Ni mara ya pili kwa Okoro kupatikana na hatia.
Mwaka 2014, alihukumiwa kifungo cha nje cha miezi 18 baada ya mwanamke kuwasilisha tuhuma za unyanyasaji wa kingono dhidi yake.
Okoro alihitimu kama daktari Lagos, Nigeria, mwaka 1986.
Previous
Next Post »