Kutokuwepo kwa Diamond kwenye birthday ya Romy Jons ambaye ni Official Dj wa Diamond na Vice President wa Wasafi kumeendelea kuchochea tetesi hizo kuwa wawili hao hawaivi.Alipoulizwa kuhusu maelewano baina yake na Diamond na kwanini Diamond hakutokea kwenye birthday yake,Romy alifunguka kwenye mahojiano yake kwenye kipindi cha Friday Night Live cha Eatv na kusema..
“Unajua hizi social networks tukizifuatilia zitakuja kutuua,ushawai kuona ndigu wanagombana?Hatuna ugomvi wowote,ninapokuwa sisafiri ujue nakuwa na majukumu mengine,WCB imekua and i’m the vice president wakati mwingine nakuwa nalinda ofisi,hakuja kwenye birthday yangu kwa sababu alikuwa ofisini lakini alitaka kuja saa mida ya saa kumi mimi nikamkatalia kwa sababu ilishakuwa late“.
ConversionConversion EmoticonEmoticon