VIDEO: Sababu za CHADEMA kuahirisha UKUTA


Siku ya kwanza ya mwezi September 2016 imekua ikitajwa sana kwenye headlines siku za karibuni na ni baada ya chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kutangaza kufanya maandamano nchi nzima, maandamano ambayo hata hivyo vyombo vya dola viliyapiga marufuku.
Leo August 31 2016 mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ametangaza kuahirisha mikutano na maandamano kwa muda wa mwezi ili kuwapa nafasi wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini kutafuta suluhu ya jambo hili kwa kukutana na Rais na Serikali yake, Mbowe amesema…..
>>>’Sisi tunawaheshimu viongozi wetu wa kidini tumekutana nao na kusikiliza wito wao wa kuahirisha UKUTA kwa wiki mbili au tatu ili wapate fursa ya kuzungumza na Rais Magufuli na Serikali yake, huu ni wito wa busara na wenye kulijali taifa letu na wajibu wake sio wito unaopaswa kupingwa kwa sababu nyepesi nyepesi’ 

Previous
Next Post »