Baada ya vipigo vitatu mfululizo, Man United kapata ushindi EFL Cup


Baada ya klabu ya Manchester United inayofundishwa na kocha raia wa Ureno kufungwa mechi zake tatu mfululizo, usiku wa Septemba 21 2016 Man United walishuka tena dimbani kucheza mchezo wao wa EFL dhidi ya Northampton.
3608
Katika mchezo huo ambao mashabiki wa Man United walikuwa na presha kubwa kama ambavyo Jose Mourinho alikasirishwa na kuwanyima mapumziko wachezaji wake, walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3-1 wakiwa ugenini.
2478
Man United ndio walianza kupata goli dakika ya 17 kupitia kwa Michael Carrick lakini lilisawazishwa dakika ya 42 na Alex Revell, kipindi cha pili Man United walikuja na kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa kitu ambacho kilifanya wapate goli la pili dakika ya 68 kupitia kwa Ander Herrera na Marcus Rashford akahitimisha kwa kufunga goli la tatu dakika ya 75.



Previous
Next Post »