Donald Trump awarai Wamarekani weusi kumuunga mkono

Donald Trump awarai watu weusi

Image captionDonald Trump awarai watu weusi
Mgombea wa urais nchini Marekani Donald Trump amezuru kanisa moja la watu weusi mjini Detroit katika jaribio la kuchukua kura za watu walio wachache kutoka kwa mpinzani wake wa chama cha Democrat Hillary Clinton.
Ameuambia umati wa watu kwamba anaelewa kwamba Wamarekani weusi wamekabiliwa na ubaguzi.
Kura za maoni zinasema kuwa Trump ambaye yuko nyuma ya bi Clinton kwa umaarufu ana ufuasi mdogo miongoni mwa Wamarekani weusi na wapiga kura wa Hispanic.
Aliandamana na Ben Carson, mgombea wa chama cha Republican ambaye alilewa katika mji huo.
Donald Trump awarai watu weusi
Image captionDonald Trump awarai watu weusi
Bwana Trump aliwasili katika kanisa hilo huku kukiwa na maandamano dhidi yake yaliofanyika nje ya kanisa hilo.
Akiwa ndani ya kanisa hilo alifanya mahojiano ya moja kwa moja na askofu Wayne T Jackson ambayo yatapeperushwa hewani .
Previous
Next Post »