Je ushawahi kupokea
simu ya dharura? Je wewe hujitenga vipi na watu waliokaribu nawe ima ni
mkeo ama hata wafanyakazi wenza ili upokee simu ya kibinafsi?
Na je katika enzi hizi za simu za kisasa au Smartphone wangapi wetu wanatumia simu za kale zisizo na touchscreen?Haya basi, Hayo sio maswali ya kipima joto ... la!
Amini usiamini Rais Yoweri Museveni, alishuka kutoka kwenye gari lake rasmi akachukua kiti chake na kukiweka kando kando ya barabara mpya ya Isingiro ikipitia kijiji hicho cha Kyeirumba hadi Tanzania na kupokea simu faraghani.
Baada ya dakika 30 hivi raia wa kijiji hicho walishangaa kuwa miongoni mwa maafisa wakuu serikalini.
Waganda katika mitandao ya kijamii wamesambaza picha hiyo ya rais museveni akizungumza kwa simu ambayo inaonekana kuwa sio ya kisasa.
''Kwani hangeweza kupokea simu yake ndani ya gari lake?"
''Ni siri gani hiyo ambayo hakutaka hata walinzi wake wasikie.
''Ama ilikuwa ni #Besigyexit?", wakizungumzia kuachiliwa kwa dhamana kwa kiongozi wa upinzani Dkt Kizza Besigye mapema asubuhi.
ConversionConversion EmoticonEmoticon