Kiongozi wa kundi
la wapiganaji la Taliban amezungumza kwa mara ya kwanza tangu
kuchaguliwa kwake mwezi mei, ambapo ameitaka Marekani kuondoka
Afghanistan.
Maulawi Haibatullah Akhundzada amesema uwepo wa
Marekani na washirika wake nchini Afghanistan hautaathiri juhudi za
makundi ya kijihadi.
Amesema kuwa Taliban haitaki kuwa na ukiritimba wa
mamlaka, japo akasisitiza kwamba ni Lazima serikali ya Afghanistan
ikatize uhusiano wake na Marekani, kama hatua ya kwanza ya mchakato wa
amani katika misingi ya sheria za kiislamu.
ConversionConversion EmoticonEmoticon