Matthew, Katrina? Vimbunga vinavyopewa majina duniani

Kimbunga Hermine

Image copyrightNASA
Umewahi kusikia vimbunga vikiwa na majina ya kushangaza, mfano cha sasa kinachoitwa Matthew ambayo kimekumba maeneo ya Haiti, Jamaica, Jamhuri ya Dominika, Bahamas na baadhi ya majimbo ya Marekani.
Mwezi uliopita kulikuwa na kimbunga kingine kilichojulikana kama Hermine ambacho kilisababisha uharibifu mkubwa jimbo la Florida.
Lakini kinachokumbukwa sana ni kile kwa jina Katrina ambacho kiliathiri sana majimbo ya Louisiana, Mississippi na Alabama nchini Marekani.
Je, vimbunga hivi hupewa vipi majina?
Uharibifu wa kimbunga HermineImage copyrightREUTERS

Vimbunga vinavyopewa majina

Vimbunga katika maeneo ya bahari ya Atlantiki, maeneo ya Caribbean na Ghuba ya Mexico hupewa majina ya Shirika la Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) ambalo lina makao yake makuu nchini Uswizi.
Zamani, ni majina ya kike pekee yaliyotumiwa lakini kuanzia 1979, majina ya kiume yalianza kutumiwa.
Huwa kuna makundi sita ya majina ambayo hutumiwa kwa mzunguko.
Hii ina maana kwamba majina yaliyotumiwa kwenye vimbunga mwaka hu hayatatumiwa tena hadi 2022.
Majina kwenye orodha hii yanaweza kubadilishwa na WMO.
Orodha hii ilianza kutumiwa mwaka 1979. Kabla ya hapo, jina la kimbunga Fern lilibadilishwa mwaka 1966 na badala yake kukatumiwa Frieda. Hakuna sababu iliyotolewa.
North Atlantic, Caribbean and Gulf of Mexico storm namesImage copyrightWORLD METEOROLOGICAL ORGANISATION

Majina yanavyoacha kutumiwa

Baadhi ya majina huacha kutumiwa, sana kunapotokea uharibifu mkubwa au hasara kubwa hivi kwamba kutumia tena jina hilo kutafufua kumbukumbu zenye uchungu.
Mfano ni kimbunga Katrina kilichoua watu 2,000 mwaka 2005 na kusababisha uharibifu mkubwa Marekani.
Kimbunga hicho kiliwaacha watu milioni moja bila makao. Mji wa New Orleans, Louisiana uliathirika sana.
Picha ya kutoka angani ya eneo la Lower Ninth Ward mjini New Orleans wakati wa mafuriko yaliyotokana na kimbunga Katrina, na nyingine ya eneo hilo miaka kumi baadayeImage copyrightAP
Image captionPicha ya kutoka angani ya eneo la Lower Ninth Ward mjini New Orleans wakati wa mafuriko yaliyotokana na kimbunga Katrina, na nyingine ya eneo hilo miaka kumi baadaye
Katika WMO kuna kundi la wataalamu liitwalo Kamati ya Vimbunga vya Tropiki ambalo hukutana kila mwaka.
Kundi hilo ndilo huamua ni majina yapi yatatumika tena na ni yapi yataacha kutumiwa.

Majina yaliyoacha kutumiwa

Kando na Katrina, kuna majina mengine ambayo yameacha kutumiwa. Mitch, kutokana na kimbunga cha mwaka 1998 kilichoua watu 11,000 Honduras na Nicaragua, halitumiwi tena. Kimbunga hicho ndicho kibaya zaidi kukumba maeneo ya Magharibi mwa dunia katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.
Tegucigalpa nchini HondurasImage copyrightGETTY IMAGES
Kimbunga Sandy cha mwaka 2012 na Kimbunga Irene 2011 pia vilisababisha uharibifu mkubwa. Majina hayo hayatumiwi tena.
Kimbunga hatari zaidi kuwahi kukumba Marekani kilitokea 1780, ambapo kiliua watu 22,000 maeneo yaMartinique, Barbados na St Eustatius.
Wakati huo majina hayakuwa yameanza kutumiwa kurejelea vimbunga.
Previous
Next Post »