Mgombea wa kiti cha
urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump, ambaye
amekuwa akishinikizwa kuchapisha malipo yake ya kodi, amejigamba akisema
ametumia sheria ipasavyo kulipa ushuru wa chini zaidi kuambatana na
sheria.
Amewaambia wafuasi wake kuwa ni jukumu lake kama
mfanyabiashara kutumia sheria za kodi kujinufaisha na wawekezaji na
wafanyakazi wake.Donald Trump aliwaambia hayo wafuasi wake wakati akiwa katika jimbo la Pueblo lililopo Colorado na kudai kuwa lilikuwa jukumu lake yeye kama mfanyabiashara kutumia vipengele vya sheria za kodi ili aweze kunufaika nazo yeye mwenyewe, wawekezaji na wafanyakazi wake.
Hivyo amesema anachukizwa sana jinsi anavyoona jinsi Marekani inavyotumia kodi.
ConversionConversion EmoticonEmoticon