Simba imemuomba msamaha Rais Magufuli 6, 2016


Siku nne baada ya waziri wa habari, sanaa utamaduni na michezo Nape Moses Nnauyekutangaza kuvifungia vilabu vya Simba na Yanga kutumia uwanja wa Taifa Dar es Salaam, leo October 6 kupitia kwa mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu hiyoHaji Manara wametangaza kuomba radhi kwa kosa lililofanywa na baadhi ya mashabiki wa.
“Naomba kuzungumza nanyi jambo mahususi ambalo nazungumza kwa niaba ya Rais wa klabu, kwa mara nyingine na kwa uzito mkubwa Rais wa klabu ya Simba, kamati ya utendaji, benchi la ufundi na wachezaji wanaomba radhi kwa Rais John Pombe Magufuli kupitia kwa waziri mwenye dhamana ya michezo Nape Nnauye”
“kwa kitendo kisicho cha kiungwana kilichofanywa na baadhi ya mashabiki wetu kwenye mchezo wa tarehe 1 October dhidi ya Yanga, tumeona kuna umuhimu wa kumuomba radhi na Rais John Pombe Magufuli na sio wa TFF  na waziri pekee rasilimali zetu zinajengwa kwa kodi zetu, serikali inatumia gharama kubwa katika kuziendesha rasilimali hizi”
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Simba na Yanga October 2 2016 zilipigwa marufuku na waziri wa habari, sanaa, utamaduni na michezo Nape Moses Nnauye kuendelea kuutumia uwanja wa Taifa Dar es Salaam kwa muda usiojulikana, kutokana na mashabiki wao kuharibu rasilimali za uwanja huo hususani kitendo cha mashabiki wa Simba kuvunja viti.
Previous
Next Post »