Rais
wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Joseph Kabila
Kabange, amewasili hapa nchini leo October 03 2016 kwa ziara rasmi ya
kiserikali ya siku tatu na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam,
Rais Joseph Kabila Kabange amepokea heshima ya kupigiwa mizinga 21 na
kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa ajili yake na baadaye
kushuhudia burudani ya vikundi vya ngoma.
Hapo kesho
October 04 2016 Rais Joseph Kabila Kabange atafanya mazungumzo rasmi na
mwenyeji wake Rais John Pombe Magufuli, ataweka jiwe la msingi la jengo
la Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na baadaye kushiriki dhifa ya
kitaifa iliyoandaliwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
About Admin MC3
This is dummy text. It is not meant to be read. Accordingly, it is difficult to figure out when to end it. But then, this is dummy text. It is not meant to be read. Period.
ConversionConversion EmoticonEmoticon