Idara ya ulinzi ya
Marekani imesema kuwa moja ya meli zake imetupa makombora ya kuonya
baada ya boti moja iendayo haraka ya Iran kuikaribia Meli ya Marekani.
Msemaji
wa Pentagon Peter Cook amesema kumekuwa na matukio kadhaa ndani ya wiki
hii ambapo meli za Iran zilifanya kile ambacho kinatafsiriwa kama
kutokuwa na usalama na ukosefu wa taaluma.Katika namna moja manuwari za Iran zimeripotiwa kuja karibu kwa zaidi ya mita mia mbili na meli za Marekani.
Amesema tabia ya Iran haikubaliki na ikizingatiwa kwamba meli ilikuwa kwenye mpaka wa maji wa kimataifa.
Waziri wa ulinzi wa Iran Generali Hosein Deh-ghan ametaarifu kwa kusema kuwa msako kama huo utaendelea ili kutoa changamoto kwa meli za kigeni zinazoingia kwenye maji ya Iran.
ConversionConversion EmoticonEmoticon