Mwanamume mmoja maskini nchini India alibebe maiti ya mkewe kwa zaidi ya kilomita 12 baada ya hospitali alimofariki kushindwa kumsafirisha kwa gari la kuwabebea wagonjwa hadi kijiji mwake.
Mke wa Dana Mjhi, Amang, mwenye umri wa 42, alifariki dunia baada ya kuugua maradhi ya kifua kikuu katika hospitali ya Ulaya, mji wa Bhawanipatna jimbo la Orissa.
Bwana Mahji alisema kijiji chake kilikuwa umbali wa kilimita 60 na hakuwa na uwezo wa kulipa gharama ya usafiri wa gari la kuwabebea wagonjwa.
Hospitali hiyo imekana madai hayo.
'Hakuna namna'
'Mwanamke huyo alilazwa hospitalini siku ya Jumanne na kufariki usiku huo huo.Bwana yake alichukua maiti hiyo bila kuwafahamisha wahudumu wa hospitali hiyo,' afisa mkuu wa afya B Brahma alisema
Bwana Majhi, anadai mkewe alifariki siku ya Juma nne usiku na kuamua kubeba mwili wake siku ya Jumatano baada ya wahudumu wa hospitali hiyo kumsihi kuondoa mwili huo.
' Nilikuwa nikiwaomba wahudumu wa hospitali hiyo wanisaidie gari nimbebe mke wangu lakini nikaambulia patupu.
Kwa sababu mimi ni maskini na nisingeweza kukodisha gari la kibinafsi sikuwa na njia nyingine ila kumbeba mke wangu mabegani.'
Mapema Jumatano , alisema alifunga mwili wa mkewe na
nguo na kuanza safari hiyo ndefu ya kuelekea kijijini huko Melghar kwa
mila na tamanduni za mwisho akiungana na mwanawe mwenye umri wa miaka
12 , Chaula.
Alitembea kwa takriban kilomita 12, ndipo watu walipoingilia kati na kumsaidia kwa gari la kubebea wagonjwa wakamfikisha hadi mwisho wa safari yake.
Shughuli ya kuchoma mwili wa mkewe ilifanyika siku ya Jumatano usiku.
Alitembea kwa takriban kilomita 12, ndipo watu walipoingilia kati na kumsaidia kwa gari la kubebea wagonjwa wakamfikisha hadi mwisho wa safari yake.
Shughuli ya kuchoma mwili wa mkewe ilifanyika siku ya Jumatano usiku.
ConversionConversion EmoticonEmoticon