Manukato yaweza kusaidia kukabiliana na uhalifu, wanasema watafiti

Manukato


Wanasayansi wamebaini kuwa kemikali zinazotengeneza manukato zinaweza kuhama kutoka kwenye nguo ya mtu mmoja hadi mwingine, hata kama wamegusana kidogo.
Harufu ya manukato inaweza kubaki kwenye nguo kwa siku kadhaa , licha ya kwamba huisha baada ya muda.
Jopo la wanasayansi hao linasema huu ni ushahidi wa msingi wa utafiti, lakini wanasema kwamba manukato yana uwezekano mkubwa wa kutumiwa kupata ushahidi wa uhalifu.
Katika taarifa yao waliyoindika katika jarida la kisayansi na haki,watafiti hao wanasema walifanyia uchambuzi harufu za manukato zinazoweza kufaa katika visa ambako kumekuwa na mgusano wa karibu wa kimwili kama vile kesi za uhalifu wa kingono.
Katika taarifa yao waliyoindika katika jarida la kisayansi na haki,watafiti hao wanasema walifanyia uchambuzi harufu za manukato zinazoweza kufaa katika visa ambako kumekuwa na mgusano wa karibu wa kimwili kama vile kesi za uhalifu wa kingono.
Mkuu wa utafiti huo Simona Gherghel, kutoka University College London, anasema : " Tulihisi kuna uwezekano mkubwa wa kutumiwa kwa manukato kwasababu wahu wengi ni watumiaji''.
''Tunafahamu asilimia 90% ya wanawake na asilimia 60% ya wanaume wanaotumia manukato kila siku'',
'' Wakati tunafahamu kuwa kazi kubwa katika katika sayansi ya kutafuta ushahidi ulio hamishwa - hadi sasa haujawahi kufanyika utafiti kuhusu kuhamishwa kwa manukato kutoka mtu mmoja kuelekea mwingine ."
Manukato ni mchanganyiko wa kemikali mbali mbali, ambazo zikichanganywa humpatia mtu binafsi harufu ya kipekee aipendayo .
Watafiti walipochunguza aina moja ya manukato ya wanaume , walibaini kuwa mchanganyiko huu wa kemikali uliweza kuhama kutoka kipande kimoja cha nguo iliyotengenezwa kwa pamba hadi kipande kingine cha nguo ya pamba.
Previous
Next Post »