Muogeleaji wa
Kichina He Zi alikuwa amepokea medali yake ya fedha katika mchezo wa
Springboard katika michezo ya Rio ya Olimpiki siku ya jumapili.
Lakini alipata zawadi nyengine wakati mpenzi wake
Qin Kai mbele ya matangazo ya runinga yaliokuwa yakipeperushwa duniani
kupiga goti moja na kumchumbia.Kwa bahati nzuri ,Qin ambaye yeye mwenyewe alishinda medali ya shaba alikubali.
''Tumekuwa wapenzi kwa miaka sita ,lakini sikudhani kwamba atanichumbia leo'',alisema.
Amesema kuwa :Vitu vingi vilileta ahadi nyingi ,lakini kitu kilichonigusa zaidi ni kwamba huyu ndio mtu ninayeweza kumuamini kwa maisha yangu yote.
Watazamaji wamesema kuwa kisa hicho cha kipekee kilitawala sherehe za kutoa medali katika michezo hiyo.
ConversionConversion EmoticonEmoticon