Baba wa miaka 28
nchini Marekani amenyoa kichwa chake na kuweka mchoro wa tatoo
unaofanana na kovu la kichwa cha mwanawe aliyefanyiwa upasuaji.
Josh
Marshall,ambaye anatoka Kansas aliingia katika shindano la kila mwaka
linaloendeshwa na shirika la hisani kuhusu saratani ya watoto na
kushinda taji la #BestbaldDad{baba mwenye kipara kizuri} wikendi
iliopita.Akikiri aliandika: Mimi na mwanangu katika hafla ya St. Baldtricks huko Wichita Kansas.
Niliwekwa tatoo ya kovu la mwanangu ili kuimarisha motisha yake.
Shindano hilo huwashirkisha watu wa familia na marafiki wa mtoto aliye na saratani.
Mwanawe alipatikana na uvimbe katika ubongo mnamo mwezi Machi.
''Mwanangu alikuwa na wasiwasi mwingi baada ya kufanyiwa upasuaji,alijihisi kama hayawani'',alisema Josh Marshal.
ConversionConversion EmoticonEmoticon