Marekani yapambana na moto wa msituni California

Wazima moto kusini mwa California nchini Marekani wanajaribu kuzima moto ambao umewalazimu mamia ya watu kuhama makwao.
Maafisa kutoka shirika shirika la Cal-Fire, wanasema kwa miundo msingi kadhaa katika eneo la Santa Barbara, imetishiwa na moto huo unaochochewa na upepo mkali.
Wataalamu wanaonya kuwa hali ya kiangazi pia imechangia moto huo kuenea zaidi hadi maeneo ya milima yaliyo jimbo la Los Angeles.
Previous
Next Post »