Mahakama moja
nchini Mexico amesimamisha uhamisho wa kiongozi wa genge linalouza
mihadarati nchini humo Joaquin "El Chapo" Guzman hadi Marekani.
Watu wawili wamewasilisha kesi mahakamni ya kupinga uhamisho huo.Mawakili wa mlanguzi huyo "El Chapo" wamepinga kuhamishwa kwake iliatumikie kifungo cha ulanguzi nchini Marekani baada ya kutoroka jela mara kadhaa akiwa nchini Mexico.
Mawakili wake wanadai kuwa hakuna ushahidi wa kumhusisha na njama ya kutoroka gerezani na wanakisia kuwa itachukuwa miaka 3 kwa kesi hizo kuamuliwa.
"El Chapo" anakabiliwa na mashtaka ya mauaji na ulanguzi wa mihadarati nchini Marekani.
Serikali ya Mexico ilikuwa imekubaliana na Marekani kumhamisha atumikie kifungo huko ilimradi tu asihukumiwe kifo.
"El Chapo" alikamatwa mwezi Januari takriban miezi 6 baada ya kutoroka gerezani akitumia njia ya chini kwa chini.
Uamuzi huo wa mahakama ya juu ni pigo kwa serikali hizo mbili na vita dhidi ya ulanguzi wa mihadarati.
ConversionConversion EmoticonEmoticon