Wabunge wa upinzani
nchini Tanzania ambao wamekuwa wakikosa kuhudhuria vikoa vya bunge kwa
karibu wiki ya pili mfululizo, hawatalipwa marupuupu yao wakati wa
kipindi hicho, hadi pake watakapoanza kuhuduria vikao.
Naibu spika
Dr Tulia Ackson alitoa tangazo hilo kaumbatanana uamuzi wa awali
ulitolewa na spika wa bunge mwaka 2008 wakati wabunge kutoka chama cha
CUF walichukua hatua ya kususia vikao vya bunge."Kama waakilishi wa watu, tunahitaka kuhudhuria shughuli za bunge badala ya kujisajili na kuondoka kufanya mambo ambayo hayana mahusiano na bunge". Alisema Dr. Tulia wakati akitoa tangazo hilo.
Wabunge kutoka upinzani wakiwemo wale kutoka vyama vya Chadema,CUF na NCCR, wamekuwa wakisusia vikao vya bunge tangu tarehe 30 mwezi Mei mwaka huu, wakati naibu spika aliwaamrisa waondoke bungeni baada ya kukiuka amri zake
ConversionConversion EmoticonEmoticon