Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosallyn Mworia, alisema uzimaji simu umehusisha simu na sio laini za simu, hivyo kuwataka wateja walioathiriwa na uzimaji huo wa simu kutokuwa na hofu juu ya kumbukumbu zilizopo kwenye laini zao, akisema zitabaki salama.
Alisisitiza kuwa pindi wakiweka laini hizo kwenye simu zisizo bandia, wataendelea kupata huduma kama kawaida na kuwataka kutunza laini zao na kwamba wahakikishe zimesajiliwa watakapoanza kuzitumia katika simu nyingine mpya.
Alitumia fursa hiyo kuwahimiza wateja kutembelea maduka yaliyopo sehemu mbalimbali nchini ili wajipatie simu halisi kwa bei ya punguzo kubwa linalomfanya mteja kumiliki simu kwa Sh 18,000 tu.
ConversionConversion EmoticonEmoticon