Waziri
Mkuu wa Zamani, Edward Lowassa ambaye pia alikuwa mgombea urais kwa
tiketi ya Chadema akiungwa mkono na vyama vya upinzani vinavyounda
Ukawa, jana alimuandikia waraka Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest
Mangu.
Waraka
huo ulijikita katika maagizo ya Jeshi hilo kupiga marufuku mikutano ya
hadhara ya vyama vya siasa pamoja na kuwashikilia na kuwahoji viongozi
wa vyama hivyo akiwemo mwenyekiti wake, Freeman Mbowe hivi karibuni.
Lowassa
alimueleza IGP kuwa amelazimika kumuandikia barua hiyo ili kuweka
kumbukumbu sahihi baada ya kupata taarifa za kuzuiwa kwa viongozi wa
Chadema kufanya mikutano wakati yeye alipokuwa nje ya nchi.
Alihoji
sababu za kiintelijensia zinazotolewa na jeshi hilo kuzuia mikutano
hiyo kwa madai kuwa limebaini kuna uwezekano wa kutokea vurugu
zimetumika ili kuhalalisha uminywaji wa demokrasia ya vyama vya siasa
kwani hata historia inaonesha vinginevyo.
“Uzoefu
wa historia unakinzana na madai hayo, kwa sababu yako matukio mengi
ambayo yamethibitisha kwamba mijumuiko ya wanasiasa wa vyama vya
upinzani, yakiwemo maandamano na hata mikutano ya hadhara yamefanyika
kwa amani,” alisema.
“Iko
mifano mingi inayoonesha kwamba tumefanya shughuli mbalimbali za siasa
kwa maana ya maandamano na mikutano ya hadhara kwa amani na pasipo
kuwapo hata ulinzi wa polisi,” alisema Lowassa kwenye waraka huo.

ConversionConversion EmoticonEmoticon